Isaiah 45:19-23

19 aSijasema sirini,
kutoka mahali fulani katika nchi ya giza;
sijawaambia wazao wa Yakobo,
‘Nitafuteni bure.’
Mimi, Bwana, nasema kweli;
ninatangaza lililo sahihi.

20 b“Kusanyikeni pamoja mje,
enyi wakimbizi kutoka mataifa.
Wale wabebao sanamu za mti ni watu wasio na akili,
wale waombao miungu isiyoweza kuokoa.
21 cTangazeni litakalokuwepo, lisemeni hilo,
wao na wafanye shauri pamoja.
Ni nani aliyetangulia kusema hili tangu zamani,
aliyetangaza tangu zamani za kale?
Je, haikuwa Mimi, Bwana?
Wala hapana Mungu mwingine
zaidi yangu mimi,
Mungu mwenye haki na Mwokozi;
hapana mwingine ila mimi.

22 d“Nigeukieni mimi, nanyi mkaokolewe,
enyi miisho yote ya dunia;
kwa maana mimi ndimi Mungu,
wala hapana mwingine.
23 eNimeapa kwa nafsi yangu,
kinywa changu kimenena katika uadilifu wote
neno ambalo halitatanguka:
Kila goti litapigwa mbele zangu,
kwangu mimi kila ulimi utaapa.
Copyright information for SwhNEN